Hans van der pluijm akiwa amevalia kinadhifu kwa ajili ya tuzo ya kocha bora ambayo anastahili lakini kakosa.
Mbwana Makata kocha aliyeiongoza Prison kwa takribani michezo 8 tu kati ya 26 na kumaliza nafasi ya 11 kati ya timu 14 ametangazwa kuwa kocha bora wa msimu uliomalizika 2014/2015.
Tofauti na matarajio ya Wengi, kocha wa Yanga, Hans van der Pluijm aliyeiongoza Yanga kwa muda mrefu hadi kutwaa ubingwa wa ligi kuu pia kuifikisha 16 bora ya kombe la shirikisho barani Afrika huku ikitolewa kwa mbinde na Etoile du sahel ameambulia patupu.
Makata alikuwa anawania tuzo hiyo pamoja na aliyekuwa kocha wa Simba, Goran Kopunovic.
Tuzo mbalimbali zinaendelea kutolewa usiku huu na wadhamini wa ligi kuu soka Tanzania bora, Kampuni ya simu ya Vodacom.
0 comments:
Post a Comment