Thursday, June 18, 2015

Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
MSANII aliyerejea na kutikisa na wimbo wa 'Mwana', Ali Kiba, amesema kung'ara kwake katika Tuzo za Muziki wa Tanzania (KTMA) 2015 kumetokana na kazi nzuri aliyoifanya na si mipango ya nyuma ya pazia kama inavyodaiwa.
Mkali huyo wa muziki wa kizazi kipya alitwaa tuzo sita katika hafla ya KTMA 2015 iliyofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani Citry jijini Dar es Salaam Jumamosi usiku akimbwaga mpinzani wake, Diamond Paltinumz aliyeambulia tuzo tatu.
Baada ya ushindi huo wa kishindo, kuliibuka maneno mengi mitaani kwamba ushindi wa Ali Kiba dhidi ya Diamond ulitokana na kubebwa.
Hata hivyo, akizungumza na waandishi wa habari mfupi baada ya kutua jijini hapa leo alfajiri akitoka Marekani Ali Kiba amepuuza madai hayo na kueleza kuwa kung'ara kwake kumetokana na kazi nzuri aliyoifanya kupitia wimbo wake wa 'Mwana'.
"Nina haki ya kutwaa tuzo nyingi hizo kutokana na kazi nzuri. Wimbo wangu (Mwana) ulikuwa mzuri na kiwango kimeongezeka," amesema Ali Kiba.
Aidha, msanii huyo amesema video ya wimbo wake wa 'Cheketua' imekamilika na itatoka ndani ya wiki hii.
"Video ya 'Mwana' ilizungumzwa tofauti na kila aliyeiangalia. Mtayarishaji wa 'Cheketua' si ytule aliyetengeneza video ya 'Mwana'. Kikubwa mashabiki wangu wategemea kitu kizuri," amesema zaidi Ali Kiba.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video