Friday, May 8, 2015

Siku chache baada ya kipa wa Yanga, Ally Mustapha ‘Barthez’ kuibiwa gari, wezi wamevamia nyumbani kwa kipa nyota wa zamani wa Simba, Juma Kaseja.
Watu hao walivamia usiku nyumbani kwa Kaseja eneo la Mbezi kwa Msuguri jijini Dar es Salaam na mmoja wao alifanikiwa kuingia hadi ndani baada ya kuvunja vioo na kukata nondo.
Akiwa ndani, mwizi huyo alifanikiwa kung’oa televisheni na kuivusha dirishani, pia akachukua vitu kadhaa vya umeme.
“Bahati nzuri Kaseja alishtuka, alipotoka nje aligundua kuna uvamizi. Akaanza kuwasaka, mwisho wezi waligundua ameamka. Yule aliyekuwa ndani alikimbia na kuruka ukuta.
“Jirani kwa Kaseja kuna askari pale alilazimika kupiga risasi ya moto na kufanya wezi hao wakimbie kama wendawazimu,” alieleza Abubakar Salum ‘Sure Boy’ ambaye ni jirani wa Kaseja.
“Taarifa zaidi muulize yeye mwenyewe Kaseja maana mimi nilienda kama jirani tu ila, wengi walijua mimi ndiyo nimevamiwa kama ambavyo wewe ulivyoniuliza.
Ingawa Kaseja hakupatikana, lakini taarifa zinaeleza hakuna kilichoporwa isipokuwa uharibu uliofanywa na wezi hao wakati wakijaribu kusaka njia ya kuingia ndani. Imeelezwa tukio hilo lilitoa saa 10 alfajiri, usiku wa kuamkia juzi.
Chanzo:Salehe Jembe

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video