Bakari Shime
STORI kubwa jijini Tanga ni tetesi za mabingwa wa zamani wa
Tanzania mwaka 1988, African Sports ‘Wana kimanumanu’ kumuwania kocha wa Mgambo
JKT, Bakari Shime.
Hata hivyo kocha Shime ‘’Mchawi mweusi’ amesema kuzungumza
na timu yoyote si jukumu lake kwasasa na
wanaopaswa kufanya kazi hiyo ni meneja wake Martin Kibua na wakala Nassor
Binslum.
“Nimshukuru Mungu kwamba niko salama, tetesi ambazo
zinasikika nimekuwa nikijibu kwa wepesi sana kwasababu mimi kama taasisi nina utawala
kwa maana ya wakala, meneja na mwanasheria wangu”. Amesema Shime na kuongeza; “Mimi
ninachojua vizuri sana ni kufundisha mpira, sikusomea masoko, biashara wala
sheria. Wapo watu wanaozunguka na huu ndio wakati wao. Mimi nimepumzika, huu
ndio wakati wao wa kufanya kazi ya kunitafutia timu na kufanya maongezi”.
“Nasikia kama anavyosikia mtu mwingine kwamba kuna African
Sports, Coastal Union, Mgambo wenyewe na timu nyingine, lakini naamini ukimpata
wakala wangu au meneja wangu anaweza kukwambia ukweli ni wapi wameanza
mazungumzo”.
Licha ya mtandao huu kumujulisha Shime kwamba meneja wake,
Martin Kibua tayari ameshasema kwamba kuna ofa mbili za Mgambo na African Sports
, kocha huyo akaendelea kushikilia msimamo wake wa kufuata uweledi.
“Taarifa naweza kuwa nayo, lakini huu ndio wakati wao wa
kufanya kazi, sitakiwa kuwasemea, sitakiwi kuzungumza kwa niaba yao, wakati
mimi nafundisha nafanya kazi yangu, naongea na vyomvo vya habari kuhusu mambo
ya ufundi, lakini wakati huu wao wanafanya kazi. Muda ukifika wataniambia kuna
ofa mbili na moja tumekubaliana nayo, tutaangalia falsafa yangu na falsafa ya
timu hiyo, wao wanapofanya mazungumzo wanafahamu kuwa mwalimu wetu ana falsafa
gani na anaweza kufanya kazi na timu gani. Huu ni wakati wa Kibuo na Binslum
kuzungumza, mimi nipo kando”. Amefafanua Shime anayeonekana kufuata uweledi
katika soka.
African Sports ni timu ya wanachama tofauti na Mgambo ambayo
inaongozwa na taasisi (JKT), je, Shime akienda huko ataweza kuhimili presha?
“Ni vizuri sana kwasababu mimi kama mwalimu nahitaji kupata changamoto
kila wakati, huwezi kufundisha timu ambayo imelala kila wakati ukatarajia
kupata mafanikio, lazima uwe na msukumo kutoka nyuma, ujue kwamba unafundisha
watu wanaotaka mafanikio. Usilale usingizi, kila wakati utafute mbinu za
kuwafurahisha, mimi siogopi timu ya mashabiki, siogopi timu yoyote, naamini
naweza kufundisha timu yoyote” Amesema Shime.
Kwa upande wake Meneja Martin Kibua amesema kweli zipo ofa
mbili kutoka kwa Mgambo wenyewe na African Sports.
“Kocha Bakari Shime ameifundisha Mgambo JKT msimu uliopita
na mkataba wake unaisha mwezi huu. Magambo Shooting nao wameonesha nia ya
kutaka kuendelea naye, lakini kama unavyojua ualimu ni kazi, tumepokea ofa
mbalimbali, tumepata ofa ya African Sports pia. Sisi tumewapa ofa ya Mgambo ili
wajitathimini. Hatujamalizana na African Sports, tupo katika mazungumzo,
tunasubiri kuona ni nani ataweza kufanya kazi na Shime”
0 comments:
Post a Comment