Beki wa Juventus Patrice Evra (kushoto) akishangilia na mchezaji mwenzake Paul Pogba baada ya kipyenga cha mwisho kupulizwa Bernabeu jana usiku Juventus ikitinga fainali ya Uefa.
PATRICE Evra amesema hana tatizo lolote na Luis Suarez, hivyo atashikana naye mkono kabla ya mechi ya fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya.
Mwaka 2012 Suarez aliwahi kugoma kumshika mkono Evra kabla ya mechi baina ya Manchester United na Liverpool uwanja wa Old Trafford na hii ilikuwa miezi minne baada mlinzi huyo raia wa Ufaransa kumtuhumu Suarez kwa ubaguzi wa rangi.
Baadaye Suarez alitiwa hatiani kwa kumbagua Evra na akafungiwa mechi nane (8) na kutozwa faini ya paundi elfu 40 kutokana na tukio hilo lililotokea kwenye sare ya 1-1 baina ya Liverpool na Man United uwanja wa Anfield mwezi Oktoba 2011.

Luis Suarez (kushoto) na Evra walirushiana maneno makali katika sare ya 1-1 baina ya Liverpool na Manchester United mwaka 2011.

Suarez alikutwa na hatia ya kumbagua Evra

Suarez alifungiwa mechi 8 na kutozwa faini ya paundi elfu 40 kutokana na tukio hilo lililotokea mwezi Oktoba mwaka 2011

Suarez alirejea uwanjani baada ya kumaliza adhabu yake na wakati huo Liverpool ilikuwa inakabiliana na Man United , Old Trafford mwezi februari 2012

Mshambuliaji wa Liverpool wakati huo, Luis Suarez aligoma kushika mkono Evra

Siku hiyo United walishinda 2-1 dhidi ya Liverpool na Evra alishangilia mbele ya Suarez.
Evra na wachezaji wenzake wa Juventus walikata tiketi ya kucheza fainali ya Uefa Champions League mwaka huu kwa ushindi wa jumla wa magoli 3-2.
Barcelona nao walitinga fainali kwa ushindi wa jumla wa magoli 5-3 dhidi ya Bayern Munich.
Alipouliza kuhusu kukabiliana na Suarez juni 6 mwaka huu, Evra alisema: "Watu wengi wananiuliza swahi hili. Sijali, kitu cha muhimu zaidi ni kwamba nitacheza fainali".
"Najivunia vile nilivyo, najivunia rangi yangu na nitamshika mkono, haina tatizo, lakini nitahakikisha anatambua uwepo wangu uwanjani.".
Suarez pia atakabiliana na Giorgio Chiellini, ambaye alimng'ata kwenye fainali za kombe la dunia mwaka jana nchini Brazil.
0 comments:
Post a Comment