MSIMU wa 2014/2015 wa ligi kuu soka Tanzania bara
umemalizika mwishoni mwa juma lililopita (Mei 9 mwaka huu) na kushuhudia Yanga
wakitangazwa mabingwa, Azam nafasi ya pili, Simba nafasi ya tatu, Mbeya City
nafasi ya nne, huku Ruvu Shooting na Polisi Morogoro zikishuka daraja.
MSIMAMO MZIMA HUU HAPA
Baada ya ligi kumalizika mtandao huu unafanya utafiti ambao
matokeo yake na maana nzima vitawekwa bayani siku za usoni, lakini umeanza na
kujua vikosi bora vya makocha wa timu za ligi kuu kwa msimu uliomalizika siku
za karibuni.
Kila kocha anapewa nafasi ya kutaja wachezaji 11 kutoka timu
zote ambao anaona wanaingia katika kikosi chake bora kabisa msimu mzima.
Leo tunaanza na kocha aliyetwaa ubingwa akiifundisha Yanga,
Hans van der Pluijm ambaye amesema;
“Golini namuweka Ally Mustafa, nadhani amecheza vizuri sana,
beki wa kulia ni Juma Abdul, mabeki wa katikati nawaweka Paschal Wawa na Nadir
Haroub, kushoto Tshabalala kutoka Simba, sijui jina lake, najua jina lake la
utani ni Tshabalala”.
“Safu ya kiungo ni Said Ndemla kutoka Simba, winga ya kulia
ni Msuva, winga wa kushoto Emmanuel Okwi, kiungo cha mbele Niyonzima na
washambuliaji wawili ni Amissi Tambwe na Kavumbagu’.
“Sikuwepo wakati ligi inaanza, nilianza kazi Yanga mwishoni
mwa mwezi Desemba mwaka jana, lakini kwa kipindi nilichoona ligi nimewaona
wachezaji hao kuwa bora zaidi msimu huu”.
KIKOSI BORA CHA KOCHA WA YANGA, HANS VAN DER PLUIJM MSIMU WA
2014/2015 NA TIMU WALIZOTOKEA WACHEZAJI HAO
1.
Ally Mustafa (Yanga)
2.
Juma Abdul (Yanga)
3.
Mohamed Hussein ‘Tshabala’ (Simba)
4.
Nadir Haroub (Yanga)
5.
Paschal Wawa (Azam fc)
6.
Said Ndemla (Simba)
7.
Simon Msuva (Yanga)
8.
Haruna Niyonzima (Yanga)
9.
Amiss Tambwe (Yanga)
10.
Didier Kavumbagu (Azam fc)
11.
Emmanuel Okwi (Simba)
Kesho tutakuletea kikosi bora cha kocha wa Coastal Union,
Jamhuri Kwhelo ‘Julio’, endelea kuwa nasi…..


0 comments:
Post a Comment