Wednesday, May 13, 2015



Na Bertha Lumala, Dar es Salaam 
'City imemaliza nafasi ya nne msimu huu ikiwa imeporomoka kwa nafasi moja ikilinganishwa na ilivyokuwa msimu uliopita.'

KAMBI ya timu ya Mbeya City imevunjwa rasmi kupisha mapumziko ya mwisho wa msimu huku nyota waliokuwa kwenye kikosi wakisafiri makwao baada ya kuwa nje na familia zao kwa kipindi kirefu.

Aidha, benchi la ufundi la City limetoa maneno ambayo yameibua hisia za timu hiyo kualikwa katika michuano ya Kombe la Kagame jijini hapa Julai mwaka huu.

Akizungumza mapema leo katibu mkuu wa City, Emmanuel Kimbe, amesema  wachezaji wote pamoja na benchi la ufundi wamepewa mapumziko hadi hapo itakapotolewa taarifa nyingine.

“Tumevunja kambi rasmi, wachezaji wanakwenda kwenye mapumziko ya mwisho wa msimu na watarejea baadaye pindi watakapotaarifiwa, hata hivyo kambi ya timu ya vijana U20 itaendelea kuwapo kwa muda wa wiki mbili zaidi, hii ni kwa sababu ya ushiriki wake kwenye michuao ya Muungano inayoendelea  hivi sasa huko Mufindi,” amesema.

Katika hatua nyingine, kocha mkuu wa City, Juma Mwambusi, amewataka wachezaji hao kutumia vizuri kipindi hiki cha mapumziko ya mwisho wa msimu ili kuwa tayari kwa mashindano yoyote yanaweza kutokea hivi karibuni.

“Kuna uwezekano wa kushiriki mashindano hivi karibuni, naomba mtumie vizuri kipindi hiki cha mapumziko mnatakiwa kujua kuwa ninyi ni kama askari kwa maana hiyo mnatakiwa kuwa tayari kwa vita wakati wowote,” amesema Mwambusi.

Maneno hayo ya Mwambusi yameibua hisia kwamba huenda timu hiyo imetaarifiwa kujiweka tayari kwa michuano ya Kombe la Kagame linalofanyika jijini Dar es Salaam Julai mwaka huu.

Pengine, City itapewa nafasi ya moja kati ya timu za Tanzania Bara (Azam FC, Yanga na Simba) endapo hazikuwa tayari kushiriki ama itakuwa miongoni mwa timu zitakazoshiriki kutokana na kufanya vizuri katika Ligi Kuu ya Bara katika misimu miwili mfululizo.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video