KAMA kuna timu ilikuwa inawakodolea macho beki wa kati wa
Azam fc, Said Hussein Mourad na kiungo Erasto Edward Nyoni kitumbua kimeingia mchanga baada
ya uongozi wa klabu hiyo kufanya maamuzi ya haraka.
Siku chache baada ya ligi kuu msimu wa 2014/2015 kumalizika, Azam imekaa
chini na kutafakari kwa kina, hatimaye imemuongezea mkataba wa mwaka mmoja
Morad ambaye alikuwa huru toka aprili 16 mwaka huu.
Katikati ya mwezi aprili mwaka huu, Mourad kupitia mtandao
huu ulitangaza kuwa huru na alikaribisha ofa kutoka timu yoyote, lakini alisema
anaipa muda timu yake ya Azam kwani bado anahitaji kufanya nayo kazi.
Hatimaye mawazo yake yamekamilika na msimu ujao ataendelea
kuvaa uzi wa Wanalambalamba.
Erasto Nyoni ambaye humudu kucheza nafasi ya beki na kiungo ndani ya Azam fc na Taifa Stars naye ameongezewa mkataba wa mwaka
mmoja.
0 comments:
Post a Comment