Neymar, Luis Suarez na Lionel Messi wakishangilia pamoja jana usiku wakati Barcelona ilipokuwa ikitafuta nafasi ya kucheza fainali ya UEFA itayochezwa Berlin juni 6 mwaka huu.
Hata hivyo Bayern wametupwa nje kwa kipigo cha jumla cha magoli 5-3, kwani mechi ya kwanza Camp Nou walifungwa 3-0 na jana wameshinda 3-2 Allianz Arena.

Mehdi Benatia akiifungia Bayern Munich goli la kuongoza katika dakika ya 7' ya mchezo na kupunguza idadi ya magoli dhidi ya Barcelona

Matumaini ya Bayern yalianza kufa dakika 8 tu baada ya kufunga goli la kuongoza kwani Neymar alifuta goli hilo

Jerome Boateng hakuwa na ubavu wa kumzuia Neymar kutia gozi kambani kabla ya mapumziko.

Robert Lewandowski (kushoto) aliisawazishia goli Bayern dakika ya 59, lakini bado wenyeji walikuwa na kazi kubwa kutokana na tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa kuwa kubwa

Thomas Muller akifunga goli la tatu na la ushindi dakika ya 74, lakini halikutosha kuwapelekea Fainali
Kusoma zaidi ingia
Follow us: @MailOnline on Twitter | DailyMail on Facebook


0 comments:
Post a Comment