Leo ni mwisho! Simba inashuka dimbani kuivaa JKT Ruvu kukamilisha ratiba ya Ligi Kuu Bara ikiwa imekosa nafasi ya pili, lakini nyota wake Emmanuel Okwi amewapoza mashabiki wa timu hiyo na kuwaahidi mambo makubwa msimu ujao.
Okwi amesema ana uhakika msimu ujao kikosi chake kitajitahidi na kushika moja kati ya nafasi mbili za juu na kushiriki michuano ya kimataifa.
“Mambo tu hayakwenda kama tulivyotarajia msimu huu, tulijitahidi kadiri ya uwezo wetu ili angalau tupate nafasi ya pili lakini ndiyo kama mlivyoona, wenzetu walikuwa wazuri zaidi.
“Nawaambia tu Wanasimba watulie ili msimu ujao tufanye kazi yetu na tutapata nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa,” alisema Okwi, raia wa Uganda.
Okwi alisema moja ya sababu za kutofanya vizuri kwa kikosi chao ni kuwa na wachezaji wengi ambao hawakuwa na uzoefu wa Ligi Kuu Bara, pia kutumia mifumo miwili ya makocha katika msimu mmoja ilikuwa tatizo.
Yanga ndiyo iliyotwaa ubingwa wa Bara na itashiriki Ligi ya Mabingwa mwakani na Azam FC imeshika nafasi ya pili na itacheza Kombe la Shirikisho Afrika.

Chanzo:Salehe Jembe

0 comments:
Post a Comment