KOCHA mkuu wa Simba aliyemaliza mkataba wake, Mserbia, Goran
Kopunovic amesema anausubiri uongozi wa timu hiyo utoe jibu kuhusu kuongezewa
mkataba wa kukinoa kikosi cha Msimbazi au la!.
Simba imedhamiria kutwaa ubingwa msimu ujao wa ligi kuu soka
Tanzania na tayari uongozi umeshaanza mipango ya kukiongezea nguvu kikosi chake
kilichomaliza nafasi ya tatu msimu huu, lakini bado hatima ya kocha wake anayeonekana
wa maana haijafikiwa.
"Kama mwanzo nilivyokueleza, ninaendelea kusubiri watasemaje. Kama
umesikia mimi ndiye nasubiriwa kutoa uamuzi, basi sawa’. Kopunovic amekaririwa
na Salehjembe akiwa nyumbani kwake nchini
Hungary . "Nimezungumza
na uongozi na kuwapa ofa yangu. Hapa ninachosubiri ni uongozi uniambie uko
tayari au la ili nije kusaini nitakuja kusaini mkataba’.
Wakati yeye
anasema anausubiri uongozi wa Simba utoe uamuzi kuhusiana na tamati yake, tayari
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe ameishasema kuwa
wameishatoa ofa kwa Mserbia huyo na wanamsubiri yeye atoe uamuzi wake.
Taarifa za
awali zilileza kwamba Kopunovic alitaka kulipwa dola 50,000 (zaidi Sh milioni
100) kwa ajili ya fedha ya usajili, jambo ambalo Simba walilikataa.
Pia
imeelezwa kwamba alitaka mshahara mkubwa ambao Simba waliona hawawezi kuulipa.
Wakati huo
huo Kopunovic, kocha mwenye msimamo ameagiza waongozwe wachezaji watatu tu
katika kikosi chake ili awape ubingwa Simba msimu wa 2015/2016 na tayari
ameshafikia maamuzi ya kuachwa kwa Danny Sserunkuma, Simon Sserunkuma na Joseph
Owino, huku akiwabakisha Emmanuel Okwi na Juuko Mursheed.
0 comments:
Post a Comment