Dennis Kitambi anakuwa kocha msaidizi namba mbili wa Azam fc.
KOCHA mkuu mpya wa Azam fc, Muingereza, Stewart John Hall amekubali
kufanya kazi na waliokuwa makocha wa muda wa klabu hiyo, George ‘Best’ Nsimbe
na Dennis Kitambi.
Nsimbe alirithi kwa muda mikoba ya, Mcameroon, Joseph Marius Omog aliyefutwa kazi mwezi
februari mwaka huu baada ya Azam fc kutupwa nje ya ligi ya mabingwa Afrika na
El Merreikh ya Sudan, wakati Kitambi naye alichukua mikoba ya aliyekuwa kocha
msaidizi, Ibrahim Shikanda.
Awali zilizuka taarifa kuwa Nsimbe na Kitambi wamepelekwa
kufundisha timu ya vijana ya akademi ya Azam fc na Stewart atakuja na wasaidizi
wake, lakini taarifa za uhakika ni kwamba makocha hao wawili wamesaini mikataba
ya kuendelea kuwa sehemu ya benchi la ufundi la timu ya kwanza.
Nsimbe amepewa mkataba wa mwaka mmoja na anakuwa kocha
msaidizi namba moja wakati kitambi naye amepewa mkataba kama huo na anakuwa
kocha msaidizi namba mbili.,
Tayari Stewart ameshaanza vikao vya ndani toka jumatatu ya
wiki hii na ataanza kazi rasmi juni 15 mwaka huu pamoja na wasaidizi wake hao.
0 comments:
Post a Comment