BAADA ya ligi kuu soka Tanzania bara msimu wa 2014/2015 kumalizika
mei 9 mwaka huu na Yanga wakiibuka mabingwa, mtandao huu unaendelea na zoezi la
kukuketea vikosi bora vilivyochaguliwa na makocha wa timu za ligi kuu na wasiokuwa
na timu pamoja na wachambuzi wa soka nchini.
Jana kocha mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm alitaja kikosi
chake bora na tukaahidi kukuletea kikosi bora cha VPL 2014/2015 cha kocha wa
Coastal Union, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’.
Katika mahojiano na mtandao huu Julio amesema kikosi chake
bora kutokana na mechi za ligi kuu alizoziona ni:
1. Ally Mustafa ‘Bartez’ (Yanga)
2. Shomari Salum Kapombe (Azam fc)
3. Paul Ngalema (Ndanda fc)
4. Juma Nyosso (Mbeya City)
5. Paschal Wawa (Azam fc)
6. Jonas Mkude (Simba)
7. Simon Msuva Yanga)
8. Salum Telela (Yanga)
9.
Amissi Tambwe (Yanga)
10.
Ibrahim Ajib (Simba)
11.
Malim Busungu (Mgambo )
Kesho tutakuletea kikosi cha Kocha wa Mbeya City fc, Juma
Mwambusi na kumbuka huyu ndiye kocha bora wa ligi kuu soka Tanzania bara msimu
wa 2013/2014 na msimu wa 2014/2015 uliomalizika mei 9 mwaka huu timu yake
imeshika nafasi ya nne huku akitajwa kuwa miongoni mwa makocha wanaowania tuzo
ya kocha bora kwa mara ya pili tena.
0 comments:
Post a Comment