Sunday, May 3, 2015

Wachezaji wa Simba SC wakishangilia kwa pamoja baada ya Ramadhani Singano kuifungia timu yao goli la pili na la ushindi dhidi ya Azam FC
Simba imefanikiwa kuifunga Azam FC kwa goli 2-1 kwenye mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara uliomalizika jioni ya leo kwenye uwanja wa Taifa na kufanikiwa kufikisha pointi 44 ikiwa nafasi ya tatu kwa tofauti ya pointi moja na Azam ambayo iko nafasi ya pili kwa pointi 45.
Ibrahim Ajib aliipatia Simba goli la kuongoza katika kipindi cha kwanza cha mchezo lakini Azam ilisawazisha goli hilo kupitia kwa Mudathir Yahya dakika za mwanzo za kipindi cha pili.
Ramadhani Singano 'Messi' (kulia) akishangilia goli aliloifungia Simba pamoja na mchezaji mwezake Ibrahim Ajib
Ramadhani Singano ‘Messi’ (kulia) akishangilia goli aliloifungia Simba pamoja na mchezaji mwezake Ibrahim Ajib
Baada ya kupata bao la kusawazisha, Azam walianza kucheza soka safi na mara kadhaa walifanya mashambulizi ya kushtukiza langoni mwa Simba lakini hawakuweza kumalizia nafasi walizo zitengeneza. Wakati Azam wakionekana kutawala soka katikati ya kipindi cha pili, ghafla Simba walibadilika na kuanza kulisakama lango la Azam kwa kufanya mashambulizi ya mara kwa mara.
Mlinzi wa Azam FC AggreyMorris akiondosha hatari langoni mwake mbele ya Emanuel Okwi
Mlinzi wa Azam FC Aggrey Morris akiondosha hatari langoni mwake mbele ya Emanuel Okwi
Ramadhani Singano ‘Messi’ akaifungia Simba bao la pili na la ushindi kwa siku ya leo baada ya mabeki wa Azam kuokoa mpira wa kona uliomkuta Singano nje kidogo ya eneo la hatari la Azam akaupiga mpira huo kwa ustadi na kuihakikishia timu yake pointi tatu.
Matokeo hayo yanaifanya vita ya nafasi ya pili inayogombewa na Simba pamoja na Azam kuzidi kuwa ngumu kutokana na tofauti ya pointi iliyopo kwa sasa kati ya timu hizo, Jumatano Azam FC itakuwa ikipambana na Yanga SC kwenye uwanja wa Taifa mechi ambayo inatarajiwa kuwa ya ushindani mkubwa kutokana na tetesi kwamba siku hiyo ndiyo Yanga watakabidhiwa kombe lao la ligi.
Kikosi cha Simba SC kilichoanza; Ivo Mapunda, Kessy Ramadhani, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ Joseph Owino, Juuko Mursheed, Jonas Mkude, Ramadhani Singano ‘Messi’, Said Ndemla, Ibrahim Ajib, Emanuel Okwi na Awadh Juma.
Walioanzia benchi; Richard Denis, Said Nassoro, Willian Lucian, Simon Sserunkuma, Abdulaziz Makame, Elius Maguri na Issa Abdallah.
Mashabiki wa Simba wakisherekea ushindi wa timu yao iliyoupata leo dhidi ya Azam
Mashabiki wa Simba wakisherekea ushindi wa timu yao iliyoupata leo dhidi ya Azam
Kikosi cha Azam FC kilichoanza; Aishi Manula, Shomari Kapombe, Gadiel Michael, Aggrey Morris, Pascal Wawa, Himid Mao, Salum Abbakar, Frank Domayo, Didier Kavumbagu, Kipre Tchetche na Brian Majwega.
Walioanzia benchi; Mwadini Ali, David Mwantika, Farid Musa, John Bocco Mudathir Yahya, Gaudence Mwaikimba na Braison Rafael

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video