Thursday, May 14, 2015


BAADA ya jana kuripotiwa kuwa kiungo mchezeshaji wa mabingwa wa ligi kuu soka Tanzania bara, Young Africans, Mnyarwanda Haruna Hakizimana Fadhil Niyonzima ameongeza mkataba wa miaka miwilli (2) kuitumikia klabu hiyo, nyota huyo amekanusha taarifa hizo katika mahojiano maalumu na mtandao huu.

Haya ndio mahojiano na Niyonzima jioni hii;

Swali: Kutoka jana kuna taarifa za wewe kusaini mkataba wa miaka miwili na timu yako ya Yanga, kuna ukweli wowote juu ya hili?

Niyonzima: Hata mimi nimekiona kitu hicho, kiukweli sijapendezwa nacho kwasababu ni uongo, mimi ni mchezaji wa Yanga na sijamaliza mkataba kama inavyotakiwa, kuna tarehe inatakiwa nifikie.

Swali: Tunajua mkataba wako upo ukingoni na kwa mujibu wa kanuni za FIFA na CAF upo huru kuzungumza na klabu yoyote ile, vipi Yanga wameonesha nia ya kukuongezea mkataba? 

NiyonzimaMaongezi na klabu yangu ya Yanga yapo, mimi sitaki kusema nitaichezea Yanga au sitaichezea Yanga, lakini ni kwamba utaratibu wote unaenda kwa njia nzuri, nimeshaongea na uongozi na kama tutafikia sehemu kwamba Haruna anasaini, kila mtu atajua, lakini kwasasa sijasaini kiukweli. 

Swali: Mkataba wako na Yanga unamalizika lini?

Niyonzima: Mkataba uko mwishoni, lakini tarehe haijafika. Namaliza mkataba wangu na Yanga Mwezi ujao. 

Swali: Inasemekana unatafuta timu nje ya nchi, je kuna ukweli juu hili?

Niyonzima: Kitu ambacho sijapenda ni  baadhi ya watu kuandika au kuchukua uamuzi kwamba nimesaini wakati sio kweli. Mimi kama nataka kwenda sehemu yoyote lazima  niiage  timu yangu ya Yanga, sijasaini timu yoyote hata Tanzania ikiwemo timu yangu ya Yanga. Mimi nipo tu kama Haruna, naamini nikifikia uamuzi wa kusaini timu yoyote au timu yangu ya Yanga, watu watajua, siwezi kusaini nikiwa nimejificha kwasababu najivunia kucheza Yanga, ni timu iliyonisaidia vitu fulani namimi nimeisaidia.


Swali: Mipango yako baada ya ligi kuu Tanzania bara kumalizika ikoje?

Niyonzima: Unajua binadamu yeyote anayetaka kuendelea au kuendeleza kipaji chake katika mpira anahitaji kwenda mbali zaidi, unahitaji kwenda sehemu ambayo mpira umeendelea zaidi kuliko hapa kwetu. Siwezi kusema malengo yangu sana kwasababu mimi sio mwenyezi Mungu, sehemu yoyote ninayoweza kuwepo Mungu ndio anajua, ila naweza kusema malengo yangu hayajatimia, niwe nimebaki hapa, niwe nimeondoka hapa, bado sijatimiza malengo yangu katika maisha yangu ya mpira.

Swali: Siku zote mara baada ya ligi kuu kumalizika, wachezaji wengi wa kigeni huondoka haraka kwenda likizo nyumbani kwao, lakini wewe bado upo Dar es salaam, ni kitu gani kimekuweka mpaka sasa?

Niyonzima: Unajua Dar es salaam tangu nimekuja kwa mara ya kwanza, nina familia yangu, nina mtoto ambaye anasoma. Huyo mtoto anatarajia kufunga masomo yake tarehe 16 mwezi wa sita. Pia watu wanajua kuwa siku za karibuni nilipata watoto, kwahiyo sio rahisi kumaliza ligi na kuondoka moja kwa moja, kuna vitu natakiwa kupanga, pia namsubiri mtoto wangu afunge shule kwasababu masomo ni muhimu kwake.

Swali: Burundi ni nchi jirani na Rwanda, sasa hivi kuna machafuko na jana imeripotiwa kuwa Rais Pierre Nkurunzinza amepinduliwa na jeshi, wewe unapata hisia gani unaposikia jambo hilo?

Niyonzima: Mimi Haruna, kitu hicho kimenipa huzuni kwasababu sisi Wanyarwanda tumeona mengi. Naweza kusema katika hii Afrika sisi tunajua vita ni kitu gani, tunajua madhara yake, nimeumia kusikia kuna watu wanauwawa, hali ya hewa sio nzuri, mimi kama binadamu naomba wahusika walete amani ili watu waishi kwa amani, sio wachezaji mpira tu, ni binadamu wote, vita sio nzuri. Watu waliopo kwenye siasa wanajua kila kinachoendelea, lakini sisi watu wa chini  hatujui cha kufanya. Tuwaombee kwa Mwenyezi Mungu ili waweze kupata amani.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video