Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
'Sserunkuma aliichezea Gor Mahia kwa mafanikio makubwa akiipa mataji ya Ligi Kuu ya Kenya (KPL) huku akiibuka mfungaji bora wa ligi hiyo msimu uliopita.'
SIKU chache baada ya kuachana na Simba, mshambuliaji Danny Sserunkuma amerejea katika klabu yake ya zamani ya Gor Mahia ya Kenya.
Hii imethibitishwa katika taarifa iliyotolewa katika mtandao rasmi wa mabingwa hao wa Ligi Kuu ya Kenya (KPL) leo.
"Gwiji wa Gor Mahia na mshambuliaji hatari Danny Sserunkuma amerejea. Taarifa kamili itafuata baadaye," ilieleza taarifa hiyo fupi iliyotolewa kama habari mahususi (Breaking News).
Dili linatarajiwa kuwa fupi huku kukiwa na taarifa kwamba mkali huyo anawaniwa na klabu za Sudan na Afrika Kusini.
Sserunkuma aliiacha Gor na kujiunga na Simba mwishoni mwa mwaka jana, akisaini mkataba wa miaka miwili lakini ameshindwa kuwaridhisha mabosi wa klabu hiyo ya Msimbazi.
0 comments:
Post a Comment