Mashabiki wa Arsenal bila shaka wanalifahamu jina la
Wellington Silva ingawa hawawezi kumueleza sana mchezaji huyo raia wa Brazil
aliyesaini mkataba Emirates mwaka 2011 kutokea klabu ya Fluminense kwa ada ya
uhamisho ya paundi milioni 3.5, lakini hakuweza kucheza England kwasababu alikosa
kibali cha kazi.
Taarifa mpya
kuhusu mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 ambaye kwasasa yupo kwa mkopo
katika klabu ya Almeria amepata uraia wa Hispania na sasa anayeruhusiwa kucheza
timu yoyote ndani ya ulaya, hivyo anaweza kuichezea Arsenal.
Wakati mashabiki wa Arsenal wakipokea kwa furaha
habari za Wellington, bado wachambuzi wa soka wanajiuliza ni jinsi gani Mbrazil
huyo atalazimisha kuingia kwenye kikosi cha Arsene Wenger kwasababu anakabiliwa
na changamoto kubwa ya kupambana na wachezaji wengine wakiwemo Alex
Oxlade-Charmberlain, Theo Walcott, Alexis Sanchez, Mesut Ozil na Serge Gnabry
na kurejea kwa Joel Campbell kunaweza kumuongezea ugumu zaidi.


0 comments:
Post a Comment