Wednesday, April 22, 2015


Na Kassim Mtolea
Timu ya soka ya Coastal Union , Wagosi wa kaya waja leo waondoka leo kutoka Tanga wameifuata timu ya Polisi huko Morogoro.

Timu hiyo imeelekea mkoani humo kupambana na maafande hao walio hoi kwenye usingizi mzito katika michezo ya ligi kuu bara,mchezo unaopigwa leo jumatano katika nyasi za uwanja wa Jamhuri huko mji kasoro.
Akizungumzia mchezo,msemaji wa wagosi wa kaya hao Oscar Assenga amesema wameifuata Polisi wakijua hali ya yao kwenye msimamo wa ligi hivyo wanatarajia upinzani mkubwa kutoka kwa maafande hao.
"Tunaamini mechi itakuwa ngumu na ugumu unaletwa na nafasi waliyopo wapinzani wetu katika ligi,watakuwa wakicheza kwa nia ya kupata pointi tatu ili waendelee kusalia kwenye ligi msimu ujao lakini sisi tupo tayari kwa mapambano"alisema.
Alipoulizwa kuhusiana na kuondoka siku moja kabla ya mchezo,Assenga alisema kuwa kwa jiografia ilivyo ya Tanga na Morogoro haiwezi kuwaathiri na watafanya vizuri leo.
"Kanuni zinatutaka tufike kituoni siku moja kabla ya mchezo ,ndio maana tunaondoka leo (jana), kwahiyo hatuna wasiwasi kabisa juu ya safari yetu kama unavyo fahamu jiografia ilivyo kati ya mikoa hii,tutafika mapema na tutafanya mazoezi pale Jamhuri"aliiambia MPENJA BLOG.
Timu hiyo ya Coastal ndio timu pekee kwa msimu huu kufungwa magoli mengi kwenye mchezo mmoja pale ilipoadhibiwa na timu ya Yanga,kwahiyo kwa sasa wanapigana kufuta aibu hiyo mbele ya mashabiki wake.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video