Dunia nzima inasubiri kwa hamu pambano la karne
baina ya Floyd Mayweather dhidi ya Manny Pacquiao.
Habari mpya leo ni kwamba Pacquiao ameonesha kuwa ana
vipaji zaidi ya vingi baada ya kuongoza na kuimba wimbo wa video alioupa jina la
‘I’m fighting for Filipinos’ yaani napigana kwa ajili ya Wafilipino.
Video ya wimbo huo ambayo tayari ameshaitoa inaonesha
umasikini wa Philipino na mataifa mengine ya bara la Asia.
Pacquiao, Mbunge mwenye miaka 36 kwa muda mredu
amekuwa akijuhusisha na siasa achilia mbali mchezo wa ngumi uliompa sifa kubwa
duniani.
Pacquiao anasubiri pambano kali dhidi ya Bondia
asiyepigika Floyd Mayweather mei pili mwaka huu Las Vegas, Marekani.
Mabondia hao wawili watacheza pambano lenye thamani ya dola za kimarekani milioni 300.
Kama Pacquiao atashinda pambano hilo, atakuwa bondia
wa kwanza kumpiga Mayweather.


0 comments:
Post a Comment