Saturday, April 11, 2015


TUNAOMBA RADHI!
KUNA taarifa imechapishwa na mtandao huu kuhusu klabu ya Simba kuwa inadaiwa katika Hoteli iliyokuwa inakaa huko Mkoani Shinyanga na ilitoka kwa dhamana 'Bondi'  kwenda Rorya kushiriki Bonanza kubwa la michezo na hatimaye kuelekea Mkoani Mwanza ambapo imefanya shughuli za kijamii jana ikitembelea kituo cha michezo cha aliyekuwa kocha wa Taifa Stars, Marehemu Sliverster Marsh.
Ripota wa mtandao huu amepotoshwa na chanzo chake kuwa lengo la Simba kupita maeneo hayo ni kupata hela za kulipa madeni na kuendesha klabu wakati huu ikiwa katika mashindano.
Kimsingi chanzo cha habari kimeonekana kuwa na nia mbaya na klabu ya Simba na kwa habati mabaya ripota naye hakwenda mbali zaidi kufuatilia habari hiyo kama taalum ya uandishi wa habari inavyomtaka.
MPENJA BLOG ni mtandao unaofanya kazi kama ofisi nyingine yoyote, kina watu wengi wanaofanya kazi za kuandika na wahariri wake, lakini kosa limefanyika kama mtu yeyote anavyoweza kukosea.
Kwa bahati mbaya habari ikishachapishwa na kusambaa ni ngumu kuifuta kichwani kwa watu, lakini muungwana siku zote anaomba radhi pale yanapofanyika makosa.
Simba ni wadau wakubwa wa Mtandao huu, tunafanya nao kazi kwa malengo mazuri ya kuiendeleza klabu hii.
Pia mtandao huu unafanya kazi na klabu zote kwa malengo ya kuendeleza soka kwa kuwajuza habari sahihi.
Kamwe hauamini katika migogoro na hautumia migogoro au uongo kwa kujitafutia umaarufu.
Lengo la kuanzishwa kwa mtandao huu ni kupasha habari zinazohusu michezo na taarifa za Simba zimekuwa zikiweka mara kwa mara kutoka kwa viongozi, wanachama na wachezaji.
Lakini lililotokea ni makosa ya kibinadamu na hii inachangiwa na baadhi ya 'Maripota' wetu kuwa na maslahi binafsi tofauti na taaluma yao. Wanafahamu taaluma inasemaje, lakini wakati mwingine wanabebwa na mapenzi.
Hili halipo katika mtandao huu pekee, ipo mingine mingi inayoandika kwa maslahi ya watu fulani. Pia vyombo vingine vimekuwa vikipotosha au kupotoshwa kuhusu mambo mbalimbali
Makosa ya ripota yanabebwa na mtandao wote. Jina la MPENJA BLOG limebeba jina la mmiliki wake, Baraka Adson Mpenja.
Kwa maana hiyo taarifa yoyote ile mbaya, iwe imewekwa na yeye au wafanyakazi wake inaibeba yeye.
Kwa niaba ya mtandao huu na ofisi yangu, mimi Baraka Adson Mpenja ninaomba radhi kwa taarifa ya upotoshaji iliyowekwa.
Kwa habati mbaya zaidi Ripota amemkariri Msemaji wa Simba, Bwana Hajji Manara, kiukweli nimesikitishwa sana na taarifa hizi ambazo chanzo chake ni mtu anayepingana na uongozi uliopo madarakani chini ya Rais Evans Aveva.
Simba ni taasisi ya watu wengi, ni timu inayopendwa na watu wengi, najua wameumizwa kwa taarifa hizi, lakini mtusamehe kwa kilichotokea.
Kwa muda wote tunawapatia taarifa rasmi kutoka klabuni na habari za mvuto kuhusu klabu, makala na uchambuzi wa mechi mbalimbali.
Kosa moja lisitufanye tuwe na uhasama! Mtandao huu unamheshimu sana Rais Aveva na viongozi wote wa Simba, kwa kutambua hilo tunaomba radhi.
Tukiwa ofsi yenye watu wenye uweledi, tunaendelea kuchukua hatua zaidi ili kumaliza tatizo.
Asante sana!

Na Baraka Adson Mpenja
Mmiliki wa MPENJA BLOG

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video