JONAS Mkude ni miongoni mwa wachezaji wenye kipaji kikubwa nchini.
Jumanne ya wiki hii, Mkude alimzika baba yake, R.I.P Faza Gerard Mkude.
Lakini kiungo huyo amezungumza na mtandao huu na kueleza jinsi alivyoachiwa na Trafiki shabiki wa Yanga baada ya kufanya kosa barabarani.
"Mpira umenisaidia sana kuongeza kipato, lakini umenifanya nifahamike zaidi kila kona ya nchi. Tena siku hizi watu wananiona kupitia Azam TV tofauti na nyuma walipokuwa wananisikia tu redioni".
"Tukienda mikoani, najisikia furaha sana ninapozongwa na mashabiki na wengine wananiita kwa nguvu, yote haya ni mapenzi yao kwangu".
"Kuna siku moja nilifanya kosa barabarani kwa bahati mbaya jijini Dar es salaam, unajua unapoendesha (gari) kuna mambo mengi yanatokea hasa kwa Dar, kuna foleni sana, unaweza ukatanua au ukachepuka, au mtu akaingiza gari na akakugonga".
"Sasa kuna siku nimefanya kosa, japo siwezi kusema ni kosa gani, Trafiki akanisimamisha na kuniamuru nipaki pembeni, nikafanya kama anavyotaka. Akanisogelea, nami nikashusha kioo, akasema oooooh! Mkude vipi ndugu yangu, wee jamaa unaniumza roho sana".
"Ujue mimi shabiki wa Yanga, daah! unakaza sana kaka. Haina noma wewe nenda, kuwa makini barabarani, alisema Trafiki huyo".
"Nikashangaa sana, kumbe umaarufu raha, lakini kuna wakati unazingua sana, unaweza kwenda sehemu kwa ajili ya starehe yako, watu wakaanza kuongea vingine". Amesema Mkude.


0 comments:
Post a Comment