SERGIO Aguero anesema Radamel Falcao "ni miongoni mwa washambuliaji wenye vipaji asilia katika soka", licha ya Mcolombia huyo kuwa katika wakati mgumu Manchester United.
Falcao alisajiliwa na United kwa mkopo kutokea Monaco mwezi septemba mwaka jana, lakini amefunga magoli manne tu katika mechi 12 za ligi kuu alizoanza, na hali hiyo imesababisha kocha Louis van Gaal akiri kutafuta suluhisho la tatizo la safu yake ya ushambuliaji.
"United ina washambuliaji wengi wenye vipaji," Aguero amewaambia waandishi wa habari."Binafsi katika maisha yangu yote ya soka namuamini zaidi Falcao"
"Amekuwa na wakati mgumu msimu huu, lakini napenda zaidi anavyojituma. Ni mchezaji mwenye ubora mkubwa. Pengine ni miongoni mwa washambuliaji wenye vipaji vikubwa zaidi vya asili"


0 comments:
Post a Comment