Friday, April 17, 2015



Na Bertha Lumala, Dar es Salaam 
'City haijawahi kuibuka na ushindi dhidi ya Yanga tangu ipande ligi kuu ya Bara msimu uliopita.'

BAADA ya kuchapwa mabao 3-1, uongozi wa Mbeya City FC umeibuka na madai mazito kwamba Yanga SC ilitumia mfuko wa nyuma kufanya vyema dhidi ya timu hiyo ya Jiji la Mbeya.

Dismas Ten, msemaji wa City, amesema  kwamba Yanga SC haina uwezo wa kuifunga timu yao kihalali ndiyo maana imekuwa ikitumia mbinu chafu kupata matokeo mazuri.

"Yanga wanatambua kwamba tuna kikosi kizuri kuzidi wao. Hawana uwezo wa kuifunga Mbeya City ndani ya Sheria 17 za Soka ndiyo maana wamekuwa wakitumia mfuko wa nyuma kupata matokeo.

"Angalia mechi iliyopita, kadi nyekundu iliyotoka dhidi ya mchezaji wetu si ya kweli. Aliyefanyiwa faulo hakuonesha dalili ya kuumizwa. Mchezaji wetu (Themi Felix) hakuwa hata na kadi ya njano kabla ya kuonyeshwa kadi nyekundu," amesema Ten.

Felix, mshambuliaji wa zamani wa Kagera Sugar FC, alilimwa kadi nyekundu na refa Mathew Akrama kutoka Mwanza dakika ya 53 kwa madai ya kumchezea rafu mbaya kiungo Salum Telela wa Yanga SC katika mechi yao ya Jumapili ya Ligi Kuu ya Bara iliyochezwa Uwanja wa Taifa jijini hapa.


Refa huyo pia alilalamikiwa na Stand United FC baada ya kuchezesha mechi yao dhidi ya Simba SC kwa dakika 100 katika kile kilichoonekana kama kuwatafutia wageni wa Uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga bao la kusawazisha katika kipigo cha 1-0, bao pekee la Mnigeria Abasirim Chidiebere.

Refa huyo aliwatoa kwa kadi nyekundu wachezaji wawili wa Stand United FC katika kile kilichoonekana pia kama kuinyong'onyesha timu hiyo pekee ya Shinyanga katika Ligi Kuu ya Bara msimu huu.

Refa Akrama pia alichezesha mechi ya watani wa jadi, Simba SC na Yanga SC iliyomalizika kwa sare ya 3-3 msimu uliopita na alifungiwa baada ya mechi hiyo kwa kutozimudu Sheria 17 za Soka.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video