Baada ya kuwepo na tetesi juu ya winga machachari wa klabu ya
Liverpool Raheem Sterling kukataa ofa ya kusaini mkataba mpya hatimaye
mchezaji huyo amethibitisha taarifa hizo.
Katika mahojiano yake jana na kituo cha Televisheni cha BBC Sterling
amesema kuwa ni kweli alikataa dili la kusaini mkataba mpya katika
klabu yake kwani yeye haihitaji pesa bali ni makombe.
Majogoo hao walimuandalia winga huyo mwenye umri wa miaka 20 mkataba
ambao ungemfanya apokee mshahara wa Paundi 100,000 kwa wiki lakini
mchezaji huyo alikataa kusaini na hivyo kuleta mashaka kwa mabosi wa
klabu hiyo
Katika mahojiano hayo mwingereza huyo alisisitiza kuwa hapendelei
pesa katika maisha yake ya soka ila kitu cha kwanza ni makombe na kwa
sasa hayupo tayari kuanzisha mazungumzo ya mkataba mpya na klabu yake
mpaka mwishoni mwa msimu huu. "Sichezi kwa ajili ya kupata
hela,ninachotaka ni vikombe.
Sichezi mpira ili niendeshe magari mazuri,niwe na nyumba nzuri. Ninachotaka ni kucheza na kushinda vikombe " alisema Sterling
Kwa upande mwingine Sterling amekanusha taarifa zilizozagaa kuwa
anataka kutimkia klabu ya Arsenal na kusisitiza kuwa taarifa hizo si za
kweli.
Winga huyo aliyejiunga na majogoo hao mwaka 2010 akitokea klabu ya
Qpr kwa sasa anapokea mshahara wa paundi 35,000 kwa wiki na amebakiza
mkataba wa miaka miwili katika klabu hiyo






0 comments:
Post a Comment