Paul Scholes amemkosoa mshambulizi wa Atletico Madrid Mario Mandzukic kwa kitendo chake cha kuwa na jazba iliyopitiliza mara baada ya kusukumwa na beki wa kulia wa Real Madrid Daniel Carvajal.
Mandzukic muda mwingi wa mchezo alionekana kuwa na jazba hasa kutokana na kukwaruzana mara kwa mara na mabeki wa Real madrid Sergio Ramos, Raphael Varane na Carvajal wakati wa pambnano hilo la ligi ya mabingwa Ulaya ambalo lilipigwa katika dimba la Vicente Calderon.
Mshambulizi huyo mwenye uraia wa Croatia alizidishwa hasira na mabeki hao kutokana na madhambi ya mara kwa mara waliyokuwa wakimchezea hasa pale alipoonekana kupigwa kiwiko na Sergio Ramos, kitendo kilichosababisha kupasuka na kuvuja damu usoni, lakini haya hivyo Scholes anasema mchezaji huyo hakutakiwa kuwa na jazba kiasi kile kwani ile ni sehemu ya mchezo tu.
Mario Mandzukic akilalamika kwa mwamuzi kuwa amepigwa kiwiko na Sergio Ramos hivyo kupelekea kupasuka na kuvuja damu usoni.

Daniel Carvajal akionekana kumg'ata na baadaye kumsukuma Mario Mandzukic

Daniel Carvajal akionekana kuusogeza mdomo wake karibu na mkono wa Mandzukic wakati wawili hao wakiwa hawana mpira.

Mwamuzi anaonekana kutoliona tukio hilo na hivyo kutochukua maamuzi yoyote.

Mandzukic akionekana kudondoka chini baada ya msuguano (tussling) kati yake na Daniel Carvajal.
'Mario alikuwa anajaribu kusababisha ugomvi usio na maana,' kiungo huyo wa zamani wa Manchester United aliiambia ITV.
'Muda mwingi wa mchezo alikuwa chini, alifanya vitu vyenye faida kwa timu mara chache sana.'

0 comments:
Post a Comment