RASHID Mandawa a.k.a ‘Kanitangaze’ msimu huu ameifungia
Kagera Sugar magoli 10 mpaka sasa, lakini mechi za karibuni amekumbwa na ukame.
Kwanini ameshuka uwezo wa kucheka na nyavu? Kocha msaidizi
wa Kagera Sugar anataja sababu zinazosababisha hali hiyo kumtokea Mandawa.
“Kuna mambo mengi yanamsumbua Mandawa (Rashid), kwanza
amekosa baadhi ya mechi kwasababu alipata kadi tatu za njano, la pili alipata
majeruhi lakini hatukuwa na jinsi kwenye
baadhi ya mechi tukalazimika kumchezesha, tunamshukuru sana kwasababu
amejitolea hivyo hivyo licha ya kuwa na majeruhi, alikuwa akipokea wito wa
kuweza kuitumikia Kagera Sugar kuhakikisha inafanya vizuri” Amesema Kabange.
0 comments:
Post a Comment