Thursday, April 16, 2015


Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
'Simba ilifungwa 2-1 nyumbani Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam dhidi ya City katika mechi ya mzunguko wa kwanza msimu huu.'

KOCHA Mkuu wa Mbeya City FC, Juma Mwambusi, ameweka wazi kuwa Simba SC haina cha kujivunia dhidi ya timu yake na dakika 90 za mchezo wao wa Jumamosi wa ligi kuu ya soka Tanzania Bara ndizo pekee zitaamua nani mbabe  tofauti na matarajio ya mashabiki wengi wa soka hivi sasa.

Kuelekea mechi mchezo huo, Mwambusi amekaririwa na mtandao rasmi wa City leo akieleza kuwa utakuwa mchezo mgumu hasa ukizingatia kuwa unazikutanisha timu ambazo kwa namna yoyote zinahitaji matokeo.

“Licha ya ubora wa kila timu, mchezo utakuwa mgumu kwa sababu kila timu inahitaji matokeo. Jambo muhimu kwetu ni kuwa tunacheza nyumbani, tutakuwa na msaada wa nguvu ya mashabiki wetu, huu ni mchezo ambao pia tumejiandaa kushinda hatuna hofu na Simba kwa sababu hawana rekodi mbele yetu,” amesema Mwambusi.
Kocha huyo ameongeza kuwa kwenye mchezo wa awali uliochezwa Uwanja wa Taifa jijini hapa Januari 28, Simba SC walikuwa na wakati mzuri kimchezo kipindi cha kwanza kabla ya kuchemsha na kukubali kichapo cha bao 2-1 baada ya dakika 90.

“Kwenye mchezo ule hakuna aliyetarajia kilichotokea, lakini sisi tulijua tunaweza kuifunga Simba ndiyo maana tuliweka bidii kubwa kipindi cha pili na kwa uwezo wa mwenyezi Mungu tukafanikiwa kupata mabao mawili, hivyo hivyo kwenye mchezo wa Jumamaosi, wengi wana imani kuwa Simba inaweza kushinda, pengine niseme kwenye soka lolote hutokea, lakini ni vigumu kwao kupata matokeo wa City  ya wakati huu”, ametamba Mwambusi.

Huu ni mchezo wa nne kwa timu hizo kukutana  katika  kinyang’anyiro cha ligi kuu ya huku City ikiwa imeshinda mara moja katika michezo mitatu iliyopita na miwili  timu hizo zikitoka sare.

Yusuph Abdalah 'Sisalo' aliyefunga bao la pili kwa mkwaju wa penalti kwenye mchezo wa kwanza msimu huu, utaukosa mchezo wa Jumamosi kufuatia maumivu ya goti  huku Hamad Kibopile aliyefunga bao la kusawazisha akiwa kwenye kikosi siku hiyo.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video