Monday, April 6, 2015


Kinara wa kufumania nyavu, Msuva atawafunga Wagosi wa Kaya?

SIMON Msuva ataiongoza Yanga katika mechi ya ligi kuu keshokutwa (Aprili 8 mwaka huu) mwaka huu uwanja wa Taifa, Dar es salaam dhidi ya Coastal Union.
Yanga iliyoitoa FC Platinum ya Zimbabwe kwa ushindi wa jumla wa mabao 5-2 na kupangiwa Etoile du Sahel ya Tunisia katika hatua ya 16 bora ya kombe la shirikisho inahitaji ushindi ili kuendelea kujikita zaidi kileleni.
Mpaka sasa Yanga inaongoza ligi kwa pointi 40 baada ya kucheza mechi 19, ikifuatiwa na Azam fc wenye pointi 36 wakiwa na mchezo mmoja mkononi.
Kuelekea katika mechi hiyo, Msuva anayeongoza orodha ya wafungaji akiwa ametia kambani magoli 11 mpaka sasa akifuatiwa na Didier Kavumbagu mwenye magoli 10 amesema ataendelea kupambana ili afunge zaidi na kujiweka katika mazingira ya kutwaa kiatu cha dhahabu msimu huu.
"Kwa misimu ya karibuni wageni wamekuwa wakifanya vizuri katika ufungaji wa magoli, msimu huu najitahidi uwe wangu. Nimefunga magoli 11 mpaka sasa, lakini lengo langu ni kufunga zaidi. Najitahidi kutumia nafasi nipatazo, kuna wakati nakosa na kupata, mpira uko hivyo".
"Didier Kavumbagu ni mfungaji mzuri wa kimataifa, nimemzidi goli moja baada ya kuongoza kwa muda mrefu, nadhani anajua nimempa changamoto, lakini lazima atambue kuwa nina nia ya kumzidi zaidi na namuomba Mungu iwe hivyo". Amesema Msuva.
Baada ya kuambiwa maneno hayo, Kavumbagu amejibu mapigo.
"Nimepata changamoto, ni kweli Msuva kanizidi, lakini bao moja kitu gani. Keshokutwa tunacheza na Mbeya City, lazima nifunge zaidi ya mawili ili nimzidi tena, baada ya hapo nitapambana mwanzo mwisho. Mfungaji lazima upende kufunga bhana" Amesema Kavumbagu.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video