Isihaka aliiongoza Simba kutwaa kombe la Mapinduzi januari 13 mwaka huu uwanja wa Amaan Zanzibar wakiifunga Mtibwa Sugar kwa mikwaju ya penalti
BEKI mahiri na nahodha wa Simba SC, Hassan Suleiman Isihaka amesema ana mpenzi wake 'kipotabo' na anampenda sana kwasababu anamuelewa wakati wote.
"Nilikuwa na mpenzi wangu wa kwanza, lakini akanimwaga kwasababu ya mipira yetu hii. Muda mwingi nipo kambini hata nikiwa nyumbani huwa nafanya sana mazoezi, sasa ikafika muda tunagombana, anaona kama simthamini kila anapotaka tuonane wakati wa kazi yangu" Amesema Isihaka.
"Nikapata mwingine, yeye anajua kazi yangu, ananipa moyo na huwa anavumilia hata nikae muda mrefu kambini".
NINI HAPENDI KATIKA MAPENZI?
Isihaka anasema: "Sipendi tabia ya kudhaniwa, unakuta mpenzi wako anakukomalia umefanya kitu fulani, umechepuka, huwa naudhika sana kwa tabia hiyo. Mimi sina hulka ya kuwa na mambo mengi, napenda kutulia nikiwa likizo"
"Sipendi michepuko babu wewee! dunia imeshaharibika"
MTANDAO GANI WA KIJAMII ANAPENDA?
Isihaka anajibu: "Zamani nilikuwa napenda facebook, lakini sasa ni mlevi wa WhatsApp. Napenda kutuma na kutumiwa mapichazi na wanangu, ni mtandao rahisi kwangu".

.jpg)
0 comments:
Post a Comment