Meneja wa timu ya Taifa ya Mexico Miguel Herrera amesema kuwa kuna
uwezekano mkubwa wa timu yake kushinda mchezo ujao dhidi ya USA licha ya
kuwa na wachezaji wengi ambao ni wachanga.
Anadai sasa hajapata timu ambayo imekomaa kiumri kwa
wachezaji wake japo anakiamini kikosi chake kuwa kitaweza kufanya
maajabu zaidi dhidi ya Marekani.
Timu hizi zitakutana siku ya kesho ambayo ni jumatano na ni
siku ambayo siyo kalenda ya FIFA na pia kikosi cha Mexico kipo katika
wakati mgumu wa kukumbwa na majeruhi wengi.
Olive Perlata na Jurgen Damm ni mojawapo ya wachezaji
walioitwa katika kikosi hicho kuwakabili Wamarekani japo hali zao za
kiafya hazipo vyema hadi sasa.
Licha ya hayo yote bado Meneja wa kikosi hicho anatamba lazima washinde...
" Kuwaleta wachezaji hawa haina maana ya kuwa wamekuja
kuonekana tu bali ni kupigania pointi 3 muhimu, tunaenda mbele zaidi
tukiwa na matarajio ya kushinda mechi na si kupoteza mchezo huo" Herrera
alisema wakati anaongea na waandishi kabla ya timu kuondoka kwenda San Antonio.
"Umekuwa kama utamaduni ambapo kila mtu anataka ashinde na
tumeongea na vijana tuliowaleta kikosini na sasa tunatarajia mambo
makubwa zaidi kutoka kwao" alizidi kusema boss huyo.
Licha ya mchezo wao na US, Mexico watakuwepo katika
mashindano ya Gold Cup pamoja na mshindi wa CONCACAF katika msimu ujao
wa majira ya joto.
Mchezo huo utachezwa hapo keshk majira ya saa mbili na nusu 8:30 usiku na utapigwa katika Dimba la Alamode


0 comments:
Post a Comment