WAKATI Cristiano Ronaldo alipiga magoli matano (5) katika mechi moja ya ligi kuu jana dhidi ya Granada, Real Madrid ikishinda 9-1, mpinzani wake Lionel Messi alishindwa kutamba mbele ya Celta Vigo jana usiku licha ya Barcelona kushinda 1-0 kwa mbinde.

Messi akimpongeza Mathieu baada ya kufunga goli muhimu
Celta Vigo waliwakazia Barca mwanzo mwisho na nyota wake watatu Luis Suarez, Lionel Messi na Neymar Jr walishinda kupenya ngome ya ulinzi ya wapinzani wao.
Ikabidi kikosi hicho cha Luis Enrique kiwageukia mabeki wake Gerard Pique na Jeremy Mathieu.

Beki wa kati raia wa Ufaransa, Mathieu alimalizia kwa kichwa mpira wa adhabu ndogo uliopigwa na Xavi na hatimaye kufanikiwa kuvunja ngome imara ya Celta Vigo.
Dakika chache kabla ya Mathieu kufunga, Pique alifanya 'takolingi' ya maana kumzua mshambuliaji wa Celta Vigo, Charles aliyekaribia kufunga goli la kuongoza.


0 comments:
Post a Comment