MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Croatia na Atletico
Madrid, Mario Mandzukic amejichora ‘Tattoo’ chini kidogo ya mgongo wake na
ilionekana jana wakati timu yake ikitoka suluhu dhidi ya mahasimu wake Real
Madrid katika mechi ya kwanza ya robo fainali ya ligi ya mabingwa uwanja wa
Vicent Calderon.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Bayern Munich
amejichora Tattoo iliyoandikwa kwa maneno ya Kiebrania yanayosomeka kwa
kiingereza “What doesn’t kill you makes you
stronger“.
Hata hivyo, Tattoo imeandikwa kutoka kushoto kwenda
kulia badala ya kutoka kulia kwenda kushoto hivyo kukosa maana na kwenda
kinyume na taratibu za grama.
Kama ingeandikwa kiusahihi ingesomeka hivi “What no to kill me, will make me stronger“, kutokana
na makosa ya kigrama.
FUNZO: Kama unataka kuandika Tattoo kwa lugha
nyingine, omba ushauri kutoka kwa mtu anayezungumza lugha hiyo kwa ufasaha.
Sasa kazi kwa nyota huyo kufuta tattoo hiyo au
kuendelea kukaa nayo milele wakati imeandikwa hovyo.

.png)
0 comments:
Post a Comment