Tuesday, April 14, 2015

Klabu ya Manchester City sasa imeamua kuweka wazi kuwa ipo tayari kuwauza Yaya Toure na Samir Nasri iwapo klabu yoyote itapeleka maombi klabuni hapo katika dirisha la usajili la majira ya kiangazi.
Taarifa hiyo imekuja siku chache tu mara baada ya City kupokea kipigo kitakatifu cha magoli 4-2 kutoka kwa mahasimu wao Mashetani wekundu timu ya Manchester United katika kinyang'anyiro cha ligi kuu nchini Uingereza.
Hapo awali ilionekana kwamba kocha wa timu hiyo Manuel Pellegrini ndiye angewajibika kutokana na matokeo hayo lakini Mabosi wa Man City wamekanusha taarifa hiyo na kusema kuwa wataendelea kuwa na meneja huyo huku wakiangalia jinsi ya kukiboresha kikosi hicho kwa ajili ya msimu ujao wa ligi
Man City wana mpango huo huku wakihofia hasara ikiwa kiungo wa timu hiyo Yaya Toure atashuka kiwango ghafla hivyo thamani yake pia kushuka. 
Nasri, naye anawekwa sokoni kutokana na sababu ya kukosa nafasi kubwa katika kikosi cha kwanza msimu huu lakini vile vile kutokana na kuonesha kiwango duni kabisa pindi walipocheza na Barcelona katika michuano ya klanu bingwa barani Ulaya. 
Mlinzi wa kushoto wa klabu hiyo Aleksandar Kolarov na mshambuliaji Edin Dzeko wote pia wapo katika hati hati ya kubaki klabuni hapo huku kiungo James Milner mkataba wake unaisha mwishoni mwa msimu huu.
Hii inaitwa oparesheni safisha safisha Man City

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video