Zlatan anajiangalia yeye zaidi kuliko timu, wakati Messi yeye anafanya kazi ya kusaidia timu kuliko kuleta 'fashion' kwenye mpira.
David Luiz kamwe sio mtu wa kumuamini.
Barca bado ni timu ya kuogopwa.
Akifanya yake: Lionel Messi akiivuruga safu ya ulinzi ya PSG kama inavyooneka.
David Luiz kamwe sio mtu wa kumuamini.
Kuna vitu vingi sana vya kupenda kutoka kwa beki huyu wa zamani wa Chelsea.
Inawezekana ikawa ni kutokana na nguvu zake akiwa uwanjani, uwezo wake mkubwa wa 'kukomand' nafasi ya kiungo.
Uwezo wake mkubwa wa kupiga mipira ya adhabu.
Ana mtindo wa nywele ambao ni kivutio kwa watu wengi.
Lakini ukweli wa mambo ni kwamba akichecheza kama beki wa kati kamwe sio mtu wa kumuamini.
Hakuwa beki wa kiwango cha ligi kuu nchini uingereza na hata alipo sasa pengine si sehemu anayostahili kuwepo.
Alifanya makosa ya kizembe wakati Dani Alves akipiga krosi ya pili na kusababisha bao, ambalo lilifungwa na Neymar, hii ilitokana na ukweli kuwa Luiz alidhani Neymar alikuwa ameotea. wakati haikuwa hivyo.

Zlatan Ibrahimovic bado si hatari katika mechi kubwa
Ukweli ni kwamba Paris Saint Germain walimuhitaji Zlatan kuipa mkali safu ya ushambuliji katika mchezo wa jana, lakini hata hivyo mambo yalienda ndivyo sivyo.
Wakati mzuri kwake ulikuwa ni pale kabla ya mchezo wakati akifananishwa na Messi kwamba nani angekuwa mwiba usiku wa jana.
Kwa mara nyingine tena wakati timu ilipokuwa inahitaji huduma yake, ndiyo wakati ambapo yeye mwenyewe haonekanai uwanjani.


0 comments:
Post a Comment