Na Bertha Lumala
"Si mara ya kwanza Yanga kutoa kipigo kikubwa cha mabao 8-0 ligi kuu kwani mwaka 1988 timu hiyo ya Jangwani jijini hapa ilitopa kipigo cha aina hiyo dhidi ya RTC Kagera (sasa Kagera Sugar) huku nyota wake Edibily Lunyamila akifunga hat trick mbili katika mechi hiyo (mabao sita peke yake).'
JANA nilieleza sababu ya kwanza ambayo ilipelekea Coastal Union FC ikumbane na dhahama ya kufungwa mabao 8-0 dhidi ya Yanga SC juzi.
Nilieleza namna Wagosi hao wa Kaya walivyofanya makosa kwa kuchezesha wachezaji wengi wa kikosi B katika mechi ya juzi huku wachezaji wenye uzoefu wakiwamo kipa Shaaban Kado, mshambuliaji Lutimba Yayo na mabeki Tumba Suedi na ndugu zake ambao hawakuwapo hata kwenye orodha ya wachezaji wa benchi la Coastal juzi.
Kwa kifupi, Coastal ilifanya makosa makubwa kuanza na kipa aliyekuwa amecheza mechi tatu tu msimu huu, Bakari Fikirini na wachezaji wengine wengi ambao hawana namba katika kikosi cha kwanza.
Pili, mtandao huu unafahamu kuwa kumeibuka makundi ndani ya Coastal Union FC tangu msimu uliopita. Tunafahamu pia kuwa kutorejea kutoka likizo kwa aliyekuwa kocha mkuu Mkenya Yussuph Chippo, kulisababishwa na makundi hayo.
Kutokana na uwapo wa figisu figisu ndani ya klabu, wachezaji nao wamejikuta wakigawanyika na kufuata maelekezo ya makundi husika.
Tatu, mabadiliko ya mara kwa mara ya benchi la ufundi pia yameiathiri Coastal Union FC ligi kuu. Coastal ndiyo timu ya Ligi Kuu ya Bara iliyonolewa na makocha wengi zaidi msimu huu.
Iliuanza msimu Septemba 20, mwaka jana ikiwa chini ya Chippo ambaye aliiongoza hadi Novemba 9, mwaka jana ligi iliposimama kupisha usajili wa dirisha dogo na michuano ya Kombe la Chalenji ambao haikufanyika, hata hivyo.
Wakati wa mapumziko hayo, Chippo alirejea kwao Kenya, lakini hakurejea jijini Tanga kutokana na kile kilichoelezwa na uongozi wa Coastal Union FC kwamba kulitokea matatizo ya kifamilia.
Lakini, wakati uongozi wa Coastal Union FC ukipotosha ukweli ukimtumia msemaji wake, Oscar Assenga, iliripotiwa na mtandao wa michezo wa futaa.com wa Kenya kwamba Chippo hakutaka kurejea Tanzania kutokana na kupata ajira nyingine ya kuwa kocha msaidizi wa AFC Leopards ya Ligi Kuu ya Kenya (KPL).
Hadi sasa Chippo ni kocha msaidizi wa AFC Leopards inayonolewa na kocha wa zamani wa Gor Mahia FC na Simba SC, Mcroatia Zdravko Logarusic.
Kutokana na kutorejea kwa Chippo, Desemba mwaka jana, Coastal Union FC ilimwajiri Mkenya mwingine, James Nandwa kuinoa timu yao. Nandwa alichemsha kuipa timu hiyo mafanikio na baada ya mechi dhidi ya Azam FC ambayo walifungwa bao 1-0 nyumbani Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga Machi 22, Nandwa aliitwa na uongozi wa Coastal na kutimuliwa muda mfupi baada ya mechi hiyo ingawa ilielezwa kwamba aliamua kuondoka mwenyewe.
Baada ya kutimuliwa kwa Mkenya huyo, kocha msaidizi wa muda, Jamhuri Kihwelo 'Julio' alipewa jukumu la kuinoa timu akiwa kocha mkuu akisaidiwa na Joseph Lazaro.
Ikumbukwe kuwa Lazaro ndiye aliyeipandisha African Sports ligi kuu msimu huu. Jambo la kushangaza ni kwamba, Lazaro alikuwa akiinoa Sports akiwa ni mwajiriwa wa Coastal Union FC.
Julio, kocha mkuu wa zamani wa Simba SC ambaye pia ni kocha mkuu wa Mwadui FC aliyoipandisha ligi kuu msimu huu, amepoteza mechi mbili mfululizo tangu akabidhiwe timu, akifungwa 1-0 nyumbani jijini Tanga dhidi ya timu iliyoko mkiani yab Tanzania Prisons FC Jumamosi kabla ya juzi kunyanyaswa kwa kipigo cha fedheha dhidi ya Yanga SC.
Wakati mabadiliko ya makocha yanafanyika, mfumo wa uchezaji pia ulikuwa ukibadilika, jambo ambalo limesababisha kuyumba kwa kikosi cha mabingwa wa 1988 wa Tanzania Bara.
ITAENDELEA KESHO

0 comments:
Post a Comment