Thursday, April 9, 2015


UTU uzima dawa! hivyo ndivyo Stand United 'Chama la wana' wanaamini baada ya kuanza harakati za kuinasa saini ya kipa wa zamani wa kimataifa wa Tanzania, Juma Kaseja.
Taarifa zilizothibitishwa na mkurugenzi wa benchi la fundi la Stand United, Muhibu Kanu zinaeleza kuwa Stand wamekusudia kumsajili Kaseja ambaye ni mchezaji huru kwasasa kutokana kwasababu uzoefu wake na uwezo mkubwa wa kudaka.
Yanga bao wakati wanamsajili Kaseja mwaka juzi walisema wanamsajili kwasababu ya uzoefu wake ili awasaidie katika michuano ya kimataifa.
Kaseja,  kipa wa zamani wa Simba alijiondoa Yanga baada ya klabu hiyo kikiuka vipengele vya mkataba, lakini Wanajangwani wamemshitaki mahakama ya kazi na kesi inaendelea kuunguruma.

Ukiangalia msimamo wa ligi kuu mpaka sasa, Stand United wanashika nafasi ya 10 wakijikusanyia pointi 24 baada ya kucheza mechi 20.
Ndanda fc na JKT Ruvu wana pointi 24 kama Stand, lakini wana wastani mzuri wa magoli ya kufunga na kufungwa.
Coastal Union waliofungwa magoli 8-0 na Yanga jana nao wana pointi 24 katika nafasi ya 11.
Kwa mazingira hayo, Stand United bado hawapo mazingira salama na wanatakiwa kukaza msuli ili kubaikia ligi kuu.
Kuanza harakati za kumsajili Kaseja ni mapema mno na wanatakiwa kujikita na mechi 6 walizobakia nazo ikiwemo mechi dhidi ya Yanga uwanja wa Taifa.
Hata hivyo jumapili iliyopita walishinda 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar Kambarage, Shinyanga.
Ushindi huo unaelezwa kuongeza morali kwa wachezaji wa timu hiyo wakiongozwa na Mnigeria, Abasarim Chidiebele mwenye magoli 7 ya kufunga.


0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video