Wednesday, April 29, 2015

KOCHA mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm amesema wembe ni ule ule katika mechi mbili za ligi kuu zilizobakia dhidi ya Azam fc na Ndanda fc.
Akizungumza na mtandao huu, Pluijm amesema katika maisha yake ya soka huwa hadharau mechi iwe inaamua hatima ya timu yake au haina athari yoyote kwa timu.
Yanga wameshachukua ubingwa  wa ligi kuu msimu 2014/2015 baada ya kuifunga Ndanda fc magoli 4-1 katika mechi ya ligi kuu iliyochezwa mwishoni mwa juma lililopita uwanja wa Taifa na kufikisha pointi 55 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote.
‘Sijawahi kuidharau timu yoyote inayocheza ligi kuu, iwe ipo juu katika msimamo au inapigana kukwepa kushuka daraja, nimebakiwa na mechi mbili, mfumo wangu ni ule ule wa kushambulia na kufunga magoli mengi, kila timu nitahakikisha naifunga kwa idadi kubwa ya magoli” Amesema Pluijm na kusisitiza: “ Wachezaji wangu sitaki wapunguze umakini kwa kuangalia timu wanayocheza nayo, heshima ni muhimu katika soka, kuchukua ubingwa haimaanishi tutafanya vibaya mechi mbili zilizosalia. Naenda Tunisia kucheza na Etoile du Sahel kisha nitarudi kucheza na Azam na Ndanda”.
Kuhusu mechi ya marudiano ya hatua ya 16 bora ya kombe la Shirikisho dhidi ya Etoile du sahel itakayochezwa Tunisia mwishoni mwa juma hili, Pluijm amesema itakuwa ngumu lakini matokeo yatapatikana uwanjani.
“Etoile wana uzoefu, wana wachezaji wazuri, lakini kama mwalimu nimeshaangalia mapungufu yao na mimi kurekebisha yangu, tutapambana kwa kushambulia muda wote, wala hatuna haja ya kujihami”.
Yanga na Etoile zilitoka sare ya 1-1 uwanja wa Taifa takribani majuma mawili yaliyopita, hivyo mabingwa hao wa Tanzania bara wanahitaji ushindi au sare ya kuanzia magoli 2-2 ili kusonga mbele moja kwa moja.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video