Monday, April 13, 2015

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Bara, Azam FC, wanaonekana kuendelea kusumbuliwa na zimwi la El Merreikh baada ya timu hiyo kushinda michezo mitatu pekee kati ya saba iliyocheza baada ya kukutana na Waarabu hao ambapo katika michezo hiyo saba imefunga mabao matatu tu.
Ipo hivi. Azam iliifunga El Merreikh mabao 2-0 Februari 15 jijini Dar es Salaam katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika na baada ya hapo ilijikuta ikiambulia sare tasa mbili kwenye mechi za ligi dhidi ya Ruvu Shooting na Prisons kabla ya kwenda kupokea kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa Waarabu hao na kuondoshwa kwenye michuano ya kimataifa.
Baada ya hapo Azam ilishinda mechi tatu mfululizo dhidi ya JKT Ruvu, Ndanda na Coastal Union ambapo zote ilishinda kwa ushindi wa mwembamba wa bao 1-0 kabla ya kukumbwa na jinamizi la sare mbili mfululizo dhidi ya Mbeya City na Mtibwa Sugar juzi Jumamosi.
Hata hivyo Azam ndiyo timu yenye rekodi ya pekee mwaka 2015 kwani haijapoteza mchezo wowote wa ligi ikiwa imeshinda mara sita na kupata sare sita katika michezo 12 iliyocheza mwaka huu. Yanga inafuatia katika rekodi hiyo ambapo imepoteza mechi moja pekee mwaka huu.
Yanga ilifungwa na Simba 1-0 pekee na imeshinda michezo tisa na sare mbili kati ya 12 ya mwaka huu.
Source: Mwanaspoti

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video