BAADA ya Kpah Sherman kufuta mkosi akifunga goli lake la kwanza katika mechi za ligi kuu Tanzania bara tangu asajiliwe desemba mwaka jana, Mbuyu Twite alimfuta kiatu chake.
Sherman alifunga goli hilo jana Yanga ikishinda 8-0 dhidi ya Coastal Union na kutoa pasi za magoli matatu.
Tukio la Twite kufuta njuma za Sherman lilifanyika kwa ustadi mkubwa na kuibua maneno kama lilipangwa au limetokea tu.

0 comments:
Post a Comment