BEKI wa kulia wa Simba, Hassan Ramadhani Kessy (katikati) akiwa na mjumbe wa kamati ya utendaji ya klabu hiyo, Amina Poyo (kushoto) na mwanachama machachari wa Simba, Bi. Hindu katika mechi ya timu ya taifa ya Tanzania ya wanawake, Twiga dhidi ya Zambia, She-polopolo iliyochezwa jana uwanja waTaifa.
Twiga Stars ilifungwa 3-2, lakini ilifuzu michezo ya wanawake ya Afrika itayofanyika mwezi septemba mwaka huu nchini Congo Brazaville kwa jumla ya magoli 6-5 kwani mechi ya kwanza nchini Zambia walishinda 4-2.
Wakati huo huo Kessy jana alipangishiwa nyumba na uongozi wa Simba na sasa anasubiri kulipwa pesa zake za usajili zilizosalia, kiasi cha milioni 5




0 comments:
Post a Comment