Kocha wa Arsenal, Mfaransa Arsene Wenger ameshangazwa
na namna chama cha soka England, FA kilivyopanga ratiba ambapo mechi kubwa ya
ligi kuu kati ya Chelsea na Manchester United itayochezwa keshokutwa itatofautiana
kwa dakika kumi na mechi ya nusu fainali ya kombe la FA.
Reading na
Arsenal zitachuana katika mechi ya nusu fainali ya kombe la FA jumamosi majira
ya saa moja dakika ishirini kwa saa za Africa mashariki na dakika kumi baadaye
itaanza mechi kubwa ya ligi kuu baina ya Chelsea na Manchester United uwanja wa
Stamford Bridge.
Wenger amesema mechi ya ligi kuu ni kubwa kwa
Chelsea na kama watapoteza mbio za ubingwa zitakuwa wazi, lakini wangependa
kuona mechi yao inakuwa ya kipekee kwasababu ni nusu fainali, hivyo
isingeingiliana na mashindano mengine.
Wakati huo huo Mfaransa huyo amekanusha taarifa za
Jurgen Klopp kuchukua nafasi yake Emirates akidai ni uzushi unaopaswa kupuuzwa
kwani bado ana mipango na timu yake.


0 comments:
Post a Comment