Kocha wa klabu ya Psg Laurent Blanc amesema timu yake ina nafasi ndogo ya kufuzu hatua ya nusu fainali katika michuano ya klabu bingwa baada ya kupoteza mchezo wa kwanza wa robo fainali.
Mabingwa hao wa Ufaransa walichezea kichapo cha 3-1 kutoka kwa Barcelona katika mchezo wa awali wa hatua ya robo fainali katika michuano hiyo uliopigwa kwenye dimba la Parc des Princes jijini Paris jumatano iliyopita.
Zlatan Ibrahimovic na Marco Verrati watakuwepo katika mechi ya marudiano ya leo baada ya adhabu zao kumalizika lakini kikosi hicho kitamkosa Thiago Silva ambaye ameungana na Thiago Motta katika wachezaji majeruhi huku David Luiz akiwa katika hatihati ya kucheza au kutocheza. "Tunatakiwa tufunge magoli, ninaamini tunaweza kufanya hivyo lakini nafasi ya kufuzu nusu fainali ni ndogo sana, Barca wanasafu nzuri ya ushambuliaji na si rahisi ukakutana nao wasifunge goli hata moja " alisema Blanc.

Mechi hiyo ya marudiano inatarajiwa kupigwa leo katika uwanja wa Nou Camp na Barcelona wataingia uwanjani wakiwa na nafasi kubwa ya kufuzu hatua inayofuata baada ya kupata ushindi wa 3-1 katika mechi ya kwanza.
0 comments:
Post a Comment