Meneja wa mabingwa wa soka barani Ulaya Real Madrid, Carlo Michelangelo Ancelotti ameridhishwa na kiwango cha kikosi chake ambacho usiku wa kuamkia hii leo kilikua na shughuli ya kuwakabili Atletico Madrid katika mpambano wa mkondo wa kwanza wa hatua ya robo fainali wa ligi ya mabingwa barani Ulaya.
Ancelotti amesema matokeo ya bila kufungana yaliyopatikana katika uwanja wa ugenini kwake sio jambo la kustaajabisha, lakini kikubwa amependezewa na jinsi wachezaji wake walivyocheza kwa kufauta maelekezo yake.
Amesema mpambano huo ulikua mgumu kwa kila upande na ana hakika hatua hiyo ilitokana na timu zote kuwa na maandalizi mazuri, lakini Ancelotti ameonesha kuwa na matumaini ya kufanya vyema katika mpambano wa mkondo wa pili ambao utachezwa juma lijalo huko Estadio Stantiago Bernabeu.

0 comments:
Post a Comment