Sunday, March 1, 2015


Na Bertha Lumala, Dar es Salaamm

Mabingwa mara 24 wa Tanzania Bara, Yanga SC wanarejea jijini Dar es Salaam usiku huu wakitokea Botswana walikoing'oa BDF XI FC katika michuano ya Kombe la Shirikisho.

Jerry Muro, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Yanga SC, ameuambia mtandao huu kuwa kikosi chao kitaingia Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere (JNIA) jijini hapa majira ya saa mbili usiku.

Muro amesema kuwa mara tu baada ya kuwasili, kikosi chao kitaunga na wachezaji wengine wanne walioachwa jijini hapa akiwano kiungo mshambuliaji Mbrazil Andrey Coutinho kuingia kambini kujiandaa kwa mechi dhidi ya Simba SC kwenye Uwanja wa Taifa jijini hapa Jumapili.

"Tunamshukuru Mungu hatuna tatizo mpaka sasa, tunarejea Tanzania kuendelea na maandalizi ya mechi mbili za VPL kabla ya kuanza maandalizi ya kuivaa Platinum ya Zimbabwe katika michuano ya kimataifa," amesema Muro.

Yanga SC imefanikiwa kutinga katika hatua ya raundi ya kwanza ya michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika baada ya kuingoa BDF XI FC kwa ushindi wa jumla ya mabao 3-2 ikishinda 2-0 jijini hapa wiki juzi kabla ya kufungwa 2-1 Uwanja wa SSKB uliopo Lobatse Km 70 kutoka Gaborone, mjini mkuu wa Botswana.

Kwa ushindi huo wa jumla, Yanga SC, mwakilishi pekee wa Tanzania katika michuano ya kimataifa mwaka huu baada ya Azam FC, KMKM na Polisi Zanzibar kung'olewa, itamenyana na Platnum ya Zimbabwe iliyoing'oa Sofapaka FC ya Ligi Kuu ya Kenya (KPL) kwa jumla ya mabao 4-2 ikishinda 2-1 Nairobi na 2-1 tena Zimbabwe juzi.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video