
LIGI kuu Tanzania bara inaendelea leo kwa mechi
tatu kupigwa katika miji mitatu nchini.
Mechi inayovuta hisia za mashabiki wengi ni ile ya
Tanga inayowakutanisha Wagosi wa Kaya, Coastal Union dhidi ya Mbeya City fc.
Msimu uliopita, Coastal waliifunga Mbeya City fc
mabao 2-0 katika uwanja huo, hivyo Wagonga nyundo hao wa Nyanda za juu kusini wanataka
kufuta uteja.
Katika msimamo wa ligi, Coastal wapo nafasi ya 7
wakijikusanyia pointi 18 baada ya kushuka dimbani mara 14.
Mbeya City wapo nafasi ya 10 wakiwa na pointi 16
kibindoni baada ya kucheza mechi 13.
Timu yoyote itakayopata ushindi itapanda nafasi
kadhaa katika msimamo ukizingatia hakuna utofauti kubwa wa pointi kwa timu zote
mpaka sasa.
Mechi nyingine za leo ni baina ya Ndanda fc na
Mtibwa Sugar uwanja wa CCM Nangwanda Sijaona Mkoani Mtwara, wakati Stand United
ipo uwanja wa CCM Kambarage, Shinyanga kuchuana na Mgambo Shootings.
Ligi hiyo itaendelea kesho kwa mechi mbili, Polisi
Morogoro wataikaribisha Simba uwanja wa Jamhuri Mkoani Morogoro, wakati Kagera
Sugar watachuana na JKT Ruvu Kambarage,
Shinyanga.
0 comments:
Post a Comment