Klabu ya Manchester City Huenda ikamuachia kiungo mshambuliaji wa klabu hiyo na timu ya taifa ya Ivory Coast Yaya Toure, kama watafanikisha kumsajili kiungo wa klabu ya Juventus Turin na timu ya taifa ya Ufaransa Paul Pogba katika usajili wa majira ya Joto.
Katika siku za hivi karibuni Yaya Toure ameonyesha kiwango cha chini akiwa na klabu yake, baada ya kutokuimarisha safu ya kiungo ya Manchester City inayoongozwa na mchezaji wa timu ya Taifa ya Uhispania David Silva.
0 comments:
Post a Comment