Na Maka Patrick Mwasomola
Hapa lazima niwe muwazi na mkweli,nimekunwa mno na mabao yote matatu ya watani zangu Dar es salaam Young Africans leo dhidi ya Mbeya City. Ni mabao makali mno,leo hakukuwa na M-Pesa katika mabao yale.
Bao la kwanza, Haruna Hakizimana Niyonzima, wenyewe mashabiki wa Yanga wanamuita Fabrigasbingawa huu ni uongo wa haki ya juu, amenikumbusha pasi aliyotoa Ramadhani Lenny Maufi kwa Edward Chumila katika uwanja huo huo na karibu sehemu ile ile na aina ya ufungaji wa goli karibia uleule, takribani miaka ishirini na tisa iliyopita, mwaka 1986 Simba ikilipa kisasi kwa Tukuyu Stars.
Nikuwepo ndani ya uwanja siku hiyo. Bao la pili najua wengi watamlaumu kipa David Baruhani lakini kwa sisi tunaoangalia kwa jicho la tatu kosa liko kwa yule kiungo aliyerudisha mpira katika umbali uke huku akiwa na uwezo wa kuupeleka mpira ule upande wa mashariki wa uwanja kutoka mahali alipokuwepo.
Ngassa! Umenikumbusha mabao yanayofungwa na wachezaji wenye akili wanaojua kutumia makosa ya wapinzani na kuwaadhibu ipasavyo! Ulikuwa na uhakika na ile cutting yako hata angekuwa Rio Ferdinand siku ile ulipokipiga na Seattle Sounders lazima angetumbukia kwenye nyavu tu.
Uokoaji wa aina ile alikuwa anaweza sentahafu wa timu ya Taifa ya Malawi peke yake Jack Loyd Chamangwana, aliwahi okoa bao kama hilo pale Shamba la Bibi Challenge Cup ya mwaka 1981 kati ya Tanzania Bara na Malawi akiokoa na miguu yake kukwama kwenye nyavu katika matokeo yale ya 2-2, ambapo Zamoyoni Mogela alibatizwa jina la Golden Boy.
Edo Kumwembe aliandika juzi kati kuwa unawezaje kumuacha striker aliyekuwa mfungaji bora akitia kambani mabao 19? Alisema anafurahi kama atakuwa anafunga tu! Na mimi namuunga mkono aendelee kufunga tu! Mara ya pili sasa namuona Amissi Tambwe akifunga mabao ya aina ile. Yanga wanajua kucheza nq akili za Simba walicheza hivi kwa striker Tambwe.
Aina ya uchezaji wa Tambwe i ule wa kuwa kama vile yupo uwani! Ni aina ya mchezaji ambaye kama katika michezo kungekuwa na mahakama za kijeshi basi viongozi wa Simba waliohusika kumuuza ingetakiwa wapelekwe court marshal na kuhukumiwa!Yanga leo wameshinda kwa uwezo wao kabisa na Mwalimu wao anajua kuusoma mchezo.
Kipindi cha kwanza Mazanda alitawala sana dimba lakini nafikiri Yanga waliona mapungufu yao wakabadilika kipindi cha pili.
Kama ningekuwa ni kiongozi katika Simba ningejipa kipindi cha miaka mitatu ya kujenga timu yenye ushindani na hii inatokana na utawala kubadili waalimu mara kwa mara.
Bado sikuona kosa la Prof. Milovan au yule Babu wa Kifaransa. Kuwaondoa waalimu katika timu kuendane na mabadiliko na mafanikio ya kweli. Yanga ni wataalamu wa maamuzi magumu! Msingemfukuza mjomba wa Coutinho ikula kwenu! Clear six points from Southern Highlands is not an easy thing! Ninawapa nafasi ya ubingwa mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment