Tuesday, February 17, 2015

MWADUI FC
Timu za Mwadui FC ya Shinyanga pamoja na African Sports ya Tanga zinatarajia kucheza mchezo wa fainali ya kusaka Bingwa wa Ligi Daraja la Kwanza (FDL) siku ya jumamosi katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

African Sports waliibuka washindi wa kwanza katika Kundi A, na Mwadui FC washindi wa kwanza Kundi B, wote watacheza mchezo huo wa fainali ambapo Bingwa atapewa zawadi ya Kombe na medali, hali kadhalika kwa msindi wa pili.

Ligi Daraja la Kwanza (FDL) ilimalizika mwishoni mwa wiki jana kwa timu nne kupanda Ligi Kuu kwa kila kundi kutoa timu mbili, Kundi A ni African Sports na Majimaji FC, Kundi B ni timu za Mwadui FC na Toto Africans.

Nazo timu za Green Worriors na Villa Squad zimeteremka Daraja la pili baada ya kushika nafasi za mwisho kwenye msimamo wa Ligi Daraja la Kwanza, Villa Squad kutoka Kundi A na Green Warriors Kundi B.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video