Friday, February 6, 2015

MABINGWA watetezi wa ligi kuu Tanzania bara wamefanya mazoezi ya mwisho jioni hii katika uwanja wa Jamhuri Mkoani Morogoro tayari kuwavaa Polisi Morogoro katika mechi ya ligi kuu soka Tanzania bara itayopigwa uwanja huo kesho jioni.
Azam waliokuwa ziarani nchini DR Congo wakishiriki kombe la Mazembe ambapo walifungwa 1-0 na TP Mazembe, wakatoka 2-2 na Zesco United ya Zambia na kufungwa 1-0 na Don Bosco watashuka dimbani kusaka pointi tatu ili kurejea kileleni mwa msimamo wa ligi kuu.
Yanga watakaochuana na Mtibwa Sugar jumapili wanaongoza kileleni wakijikusanyia pointi 22, moja zaidi ya Azam waliopo nafasi ya pili, lakini Wanajangwani wamecheza mechi 12 wakati Wanalambalamba wamecheza mechi 11.
Mechi nyingine za kesho ligi kuu ni baina ya JKT Ruvu dhidi ya Mbeya City fc uwanja wa Azam Complex, Chamazi.
Coastal Union itachuana na Simba uwanja wa Mkwakwani Tanga, wakati Ndanda fc itakuwa nyumbani Nangwanda Sijaona kukabiliana na Stand United.
Kagera Sugar itaikaribisha Mgambo JKT uwanja wa CCM Kirumba, wakati Tanzania Prisons itakuwa Sokoine kuvaana na Ruvu Shootings.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video