
Mpambano mkali wa mchezo wa masumbwi mkali utakaokutanisha mabondia mbalimbali kutoka kila kona ya Tanzania utafanyika
October 25 katika ukumbi wa friends Corner manzese jijini Dar es salaam akizingumza na waandishi wa habari mratibu wa mpambano huo kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D'
amesema kuwa siku hiyo kutakuwa na mpambano wa mahasimu katika mchezo wa ngumi kati ya bondia Saidi Mbelwa 'Moto wa Gesi' na George Dimos mpambano mwingine utawakutanisha Amani Bariki 'Manny Chuga' na Ally Bugingo mpambano unaosubiliwa kwa hamu kila kona ya jiji la Dar es salaam ambapo mabondia hawo wamejizolea umaarufu mkubwa kupitia mchezo huo
pambano jingine ni kati ya Juma Fundi atakaezichapa na Hamza Mchanjo wakati Hasani Mandula ataonyeshana kazi na Mohamedi Jaka na Shabani Kaoneka atazipiga na Ibrahimu Maokola anaejiandaa kuwania kucheza ubingwa wa taifa mwishoni mwa mwaka huu Fadhili Boika atazipiga na Godfrey Silver na Habibu Pengo atazidunda na Abdallah Luanje, Kashinde Mohamedi atazidunda na Mohamed Kibaga wakati Sadiki Nuru atakumbana na Mohamed Mbishi
![]() |
0 comments:
Post a Comment